Thursday, July 25, 2013

Tahadhari

Amyna naamini ni mzima wa afya na unaendelea vyema na mfungo mtukufu wa ramadhan.
Tafadhali publish ujumbe huu ili kila mtu awe na tahadhali na wizi ulio ibuka sasa na unaendelea kwa kwasi hapa jijini
 
Kuna taarifa ya utapeli hatari umeingia mjini watu wanajifanya wanauza manukato (Perfumes).
Watakushawishi unuse kipande cha karatasi ambacho kimenyunyuziwa dawa yenye sumu – wao watakwambia Perfumes wanayo taka kukuuzia ndio wamepulizia hapo wwe utaamini na kunusa ili usikilize harufu yake kumbe sio manukata hayo ni kitu ningine ambayo ukinusa  tu unaweza kujikuta umepoteza fahamu na hapo unawapa nafasi ya kukuibia ulicho nacho.
Tafadhari kuwa mwangalifu unapokutana na watu kama hao. Tafadhali wafahamishe ndugu, jamaa na rafiki habari hii na wote tuwe makini pindi unapo kutana na kitu kama hicho.

Asante Fatma ujumbe nimeupata na ndio huo nimeufanyia kazi.
Ramadan Kareem na Siku Njema.

14 comments:

  1. Heeeeee makubwa haya jamani mbona watatuuwa.

    ReplyDelete
  2. Ni nini hiki jamani watanzania??
    Huku tunako elekea sasa ni kubaya zaidi.

    Asante Amy

    ReplyDelete
  3. Uwiii twafa sasa iyo kitu mdogo wangu juzi kakutana nayo maeneo ya posta ya zamani salama yake rafiki yake alipita na kumpa lift ya gari other wise nahisi hili lingemkuta na yeye.

    Asante sana mamii, siku njema kwako na ramadhan Mubarak.

    ReplyDelete
  4. mmmh majanga jamani ni nni hiki, kwani watu tunashindwa kujituma na kufanya kazi kwa bidiii mpaka tukabana na kuibiana tena mbaya zaidi wengine huumizwa vibaya.

    Ndio maana me nikiona mwizi anapigwa wala hua sina huruma nao. Tuacheni hizi tabia mbaya, kesho kwa mungu kuna moto jamani.
    Me yangu ni hayo tu.

    ReplyDelete
  5. hivi nyie wezi, vibaka kwa ujumla wenu hamna kazi nyingize za kufanya ambazo zitawaingizia kipata kihalali mpaka mkakabe, mkatapeli, kuzurumu na mambo kama hayo ndio mpate hela. Am sure mnajua co vizuri na mnawaumiza watu.
    Ila kumbukeni za mwizi ni cku 39 ya 40 utajikuta kwenye mikono ya wananchi wenye hacla kali mbona utajua kama mchicha ni mboga ama majani.

    Asante mwaya kwa kutujuza ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  6. Nikisema dunia imeisha sizani kama nitakua nakosea. Jamani nduguzangu hii dunia imeisha....., mambo gani haya sasa maana kila siku tunasikia jipya yani hawa vibaka sijui wezi wenyewe kila wakilala ama kila walifanyalo hua wanafikiria na kutunga mbinu mpya tu za kufanya matukio ya huwalifu kuwaibia watu na kuwarudisha watu nyuma.

    Mna tukwaza sana sema basi tu ni vile kwenye msafara wa mamba na kenge pia wamo.

    ReplyDelete
  7. Tumuombe mungu atuepushe na haya mabalaa yanayo ibuka usiku na mchana. In Sha Allah mwenyezi mungu yupo nasi.

    ReplyDelete
  8. watu jamani muache kupenda urahisi wa kununua vitu vya mikononi kwani maduka hamuyajui yalipo!!! ndio mnakomeshwa hivyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Frank umesema point kwani maduka yanayo uzwa manukato hamuyajui yalipo eeeh. Ndio mkomesho huo.

      Delete
    2. Mnayataka wacha wayakute. Maduka yote yanayo uza perfume yalivyo mengi mpaka vichochoroni huko mnashindwa kweli kwenda kununua mpaka mungaike na zamikononi, ndio kupenda urahisi au?? ndio mnakomeshwa hivyo puuuuuuuu

      Delete
  9. kwani ndugu zangu hakuna kazi nyingine za kufanya mpaka muibe, mkabe watu, mumwagie watu tindikali na kuwapola ka kazi zote za aina iyo. Kumbukeni damu ya mtu ni nzito sana na mungu anaona matendo yenu. One day mtakiona.

    ReplyDelete