Monday, July 29, 2013

Mbaazi za kupaka

Mahitaji
ü  Mbaazi mbichi au Mbaazi kavu - ½ kl                           
ü  Kitunguu maji - Kikubwa kimoja 1
ü  Kitunguu swaum – Kiasi cha punje nne/tano
ü  Karoti – Moja kubwa
ü  Pili pili hoho – Moja kubwa
ü  Chumvi - Kiasi
ü  Manjano - ½ Kijiko cha chai
ü  Mafuta ya kupikia (Vegetable oil) – Kijiko kimoja  cha chai
ü  Pilipili mbichi – Moja moja nzima
ü  Nazi (Coconut nature) – Tatu kubwa 
ü  Giligilan
ü  Unga wa ngano (Plain flour) – kijiko kimoja cha chakula

Matayarisho na kupika
Hatua ya kwanza:
ü  Osha mbaazi kwenye chungio na ziache zitoke maji.
ü  Chambua kitunguu maji chako, kisafishe na ukikate vipande vidogo vidogo katika shape nzuri .
ü  Chambua kitunguu swaum vyako vitwange mpaka vilainike vizuri.
ü  Osha karoti na pili pili hoho kisha uvikate vidogo vidogo katika shape nzuri
ü  Kuna nazi (coconut nature) yako vizuri iwe laini na uichuje matui mawili, tui bubu(tui la kwanza) na tui la pili.

Kupika kwa mbaazi mbichi
ü  Chemsha mbaazi zako mbichi kwa maji hadi ziive lakini zisirojeke ziwe ngumu kidogo.
ü  Chukua tui lako la weka kwenye mbaazi zako pamoja na mchanganyiko wa karoti na nk.
ü  Weka tena jikoni vichemke na mpaka tui lako likauke kabisa.
ü  Mimina mbaazi zako kwenye trei ili zipoe na ni vyema zikapoa kabisa ili tui lako ukija kumwagia juu lisiyeyuke.
ü  Chukua tui lako bubu weka jikoni, weka kijiko cha chakula plat unga wa ngano (Plain flour).
ü  Koroga bila ya kuacha hadi tui lako lichemke, kisha koroga manjano yako kwenye kikombe weka kiasi.
ü  Changanya kwenye tui lako unalo lipika akikisha tui lako lina kua zito zito.
ü  Ipua na pooza kodogo tui lako.
ü  Mwagia juu ya mbaazi ukiwa unasambaza kama icesugar kwenye cake.

Kupika kwa mbaazi kavu
ü  Chambua mbaazi na kutoa uchafu osha na loweka mbaai zako usiku kucha.
ü  Mbaazi zina tabia ya kunyonya maji hivyo basi weka kwenye kikubwa na ujaze maji
ü  Asubuhi zitoe kwenye maji na ubadike jikoni weka maji hadi zitakapo anza kuiva
ü  Punguza moto ili ziive kwa moto mdogo ili zisi pasuke.
ü  Chuja nazi na tui bubu weka pembeni tumia lile tui la pili.
ü  Hilo tui la pili weka kwenye mbaazi zako pamoja na mchanganyiko wako wa vitunguu maji, hoho na nk.
ü  Weka tena jikoni ili hilo tui la pili na mchanganyiko wako uchanganyike na tui lako liivi na likauke.
ü  Ipua na umimine kwenye trei wacha zipoe.
ü  Chukua tui lako bubu weka jikoni, weka kijiko cha chakula plat unga wa ngano (Plain flour).
ü  Koroga bila ya kuacha hadi tui lako lichemke, kisha koroga manjano yako kwenye kikombe weka kiasi.
ü  Changanya kwenye tui lako unalo lipika akikisha tui lako lina kua zito zito.
ü  Ipua na pooza kodogo tui lako.
ü  Mwagia juu ya mbaazi ukiwa unasambaza kama icesugar kwenye cake.
ü  Na baada aya hapo mbaazi zako zitakua tayari kwa kuliwa

Kumbuka:
kuanza maandalizi mapema ili tui ligande kwenye mbaazi zako.
Unaweza kulia na chochote kile, iwe chapati, wali, maamri (maandazi),vitumbua yani raha tupu.

Pishi:
Limetetwa kwenu na bidada Sware Kaku. Asante sana mama naenda fanyia kazi hii kitu.
Ramadan kareem na siku njema kwetu sote In Sha Allaah. 

5 comments:

 1. Mmmh Mashaallah umenikumbusha mbali wwe mtoto. Hicho kitu sikajitia mdomoni katambo sana.

  ReplyDelete
 2. Asalaam Aleykum Madam.
  Hope swaum inapanda au sio.....
  Aisee mbaazi za kupaka zinapanda sana na chapati...uwiiiii utamu wa aje sasa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Naungana nawe mdau Sabrina. Jamani hii kitu upate na chapati hapo au wali wa nazi. mmmmmh mpaka mate yananitoka hapa.

   Asante madam kwa kunikumbusha hii kitu

   Delete
 3. umenikumbusha kwetu walai..lol

  ReplyDelete