Wednesday, September 02, 2015

TUJIFUNZE JINSI YA KUJIOKOA IKITOKEA DHARURA YA MOTO NDANI

Image result for moto unaowaka

ASANTE SANA MDAU ULIYESHEA...MUHIMU KUSOMA HII WADAU..
 
Ikiwa siku ya chache baada ya tukio la kusikitisha la kuteketea moto kwa watu 9 wa familia pale Buguruni, D'Salaam, vifuatavyo ni vitu vya kujifunza (few tips to learn) inapotokea dharura ya moto ndani ya nyumba:
 
1.     Kitu cha muhimu ni kutoka nje salama haraka iwezekanavyo (as soon as possible).
 
2.     Hakikisha (ensure) kila siku mlango wa dharura (emergency exit) ya nyumba ni umekaa kwa urahisi iwezekanvyo (as simple as possible). Kila mtu ajue funguo za milango ya kutokea zinapowekwa, sio zinafichwa balaa. Have an ermegence exit whenever possible.
 
3.     Fahamu kwamba ktk matukio mengi ya moto (in most cases) kinachoua ni moshi kabla ya moto, hivyo ukiona dalili ya moshi hakikisha unakuwa na kitambaa kibichi cha kujifunika puani na mdomoni, na kama moshi umeanza kuingia ulipo tambaa chini (crawl down) sababu hewa ya uhai (oxygen) ina uzito (density) kubwa kuliko hewa ya kifo (carbon monoxide) hivyo inakuwa imekandamizwa chini sentimita chache kutoka kwenye sakafu (few centimeters from the floor). Hivyo tembea kwa kutambaa.
 
4.     Hakikisha unawajulisha watu wote (Ensure you alert everybody) kama wamelala ili waweze kutoka nje haraka.
 
5.      Achana na fikra ya kuokoa vitu, ktk hatua hii cha muhimu ni kuokoa uhai kwanza.
 
6.      Kumbuka, muda ni kitu cha msingi, fanya haraka iwezekanavyo (quick as possible) katika kujiokoa na kuokoa wengine.
 
7.     Ni muhimu nyumba zetu kuziwekea kiashiria moshi (smoke detectors) na pia kizima moto (fire extinguishers). Kugundua haraka (early detection) ya moto ni muhimu sana ili kuweza kuudhibiti kirahisi. Smoke detector ni mashine ya elektroniki ambayo inagundua moshi ktk hatua ya mwanzo kabisa na itapiga kelele (alarm) kwa sauti ya juu, itakusaidia kuamka hata kama upo usingizini na kuweza kujiokoa na kuokoa wengine na kuuzima moto kabla hujashika kasi.
 
 
Shukrani na sambaza ujumbe huu kwa wengine