Friday, February 28, 2014

Al Jumaa Maqbur


Salamu za Ijumaa kwa dhati nakutumia. Furaha imenikaa na dua nakuombea.
Mola akupe shifaa na moyo ulotulia. Rabbi akujaze twaa, upate kuong'okewa.
Kila lenye manufaa njia kukunyooshea. Akulinde na balaa, kheri kukumiminia.
 
"AL JUMAA MAQBUR".

Wednesday, February 26, 2014

Cake Mguso




Cake Mguso.....lol
Guys iyo kitu hapo juu kimenigusaje sasa nikaona nooo let me share with you.
Credit: Bella Naija.

Saturday, February 22, 2014

Matokeo ya Mtihani wa Taifa kidato cha nne - 2013



Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne wa 2013, huku ufaulu ukiongezeka kwa 15.17%. 
Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji ambao ulipanua wigo wa alama na madaraja, hivyo kutoa nafasi kubwa zaidi kwa watahiniwa kufaulu. 
Licha ya kuanza kutumika kwa mfumo huo mpya, idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwani watahiniwa 151,187 sawa na 42.91% wamepata sifuri. Kati ya hao, wavulana ni 78,950 sawa na 41.54% na wasichana ni 72,237 sawa na 44.51%.  
 Fungua hiyo link kunionea http://41.188.155.122/CSEE2013/olevel.htm



Thursday, February 20, 2014

Anusurika kuuwawa na Chui - China

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/18/140218101721_tiger_man.jpg
Mwanamume mmoja nchini China amenusurika kifo katika hifadhi ya wanyama pori nchini humo, baada ya kujirusha ndani ya hifadhi hiyo akisema alitaka 'kuwalisha' wanyama hao hatari.

Mwanamume huyo alitaka kujitoa uhai kwa kujirusha ndani ya chumba cha kuhifadhia Chui wakubwa wenye Milia au Tiger katika hifadhi ya wanyamapori nchini China. Wageni waliopigwa na mshangao, walitizama mwanamume huyo aliyejulikana kama Yang Jinhai, mwenye umri wa miaka 27 akiumwa, kugwaruswa na kubururwa na wanyama hao kabla ya walinzi kumuokoa.
 
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la China, Chengdu, watalii waliokuwa katika hifadhi hiyo walidhani kuwa bwana Yang alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa hifadhi hiyo kwani walioshuhudia wanasema walimuona akibeba begi mabegani na kupanda mti kama aliyetaka kuwalisha wanyama hao wakubwa. 
Lakini baada ya watalii kuanza kumpigia mayowe wakimtaka arejee, bwana Yang alijirusha kutoka mtini na kuanguka ndani ya sehemu walimokuwa wamefungiwa Chui hao.
Watalii hao walisema kuwa Yang alijirusha akitaraji kuwa Chui hao wangemshambulia na kumuua , lakini wanyama hoa waliokuwa Chui Milia Dume na Jike walionekana kushtuka zaidi kwa kumuona Yang huku Chui jike akitoroka kuliko kutaka kumla Yang.
 
Bwana Yang alionekana akijaribu kuwafanyia vitendo vya kuwakasirisha ili wanyama hao waweze kumshambulia lakini hakufanikiwa. Hatimaye Chui Dume alimshambulia Yang baada ya kushikwa na hasira na kuanza kumuuma na kumgwara lakini aliokolewa na walinzi wa hifadhi hiyo.

Yang alipata matibabu lakini baada ya kutibiwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa nia yake ilikuwa 'kuwalisha wanyama hao. Familia ya Yang ilisema kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili na kuwa walikuwa wamepanga kumpeleka hospitalini kwa ushauri nasaha.

Walinzi wa hifadhi hiyo walisema kuwa Yang alikuwa na bahati mno kuweza kunusurika kifo.
Kwa msaada wa BBCSwahili.com