Wednesday, April 16, 2014

African Print


Hey beautiful people. I hope that you’re well.
Another style of African Print.

 Source: Vlisco.com

Monday, April 14, 2014

R.I.P Nguromo

Innalilah Wainnailahi Rajooun. Hii ni safari ya kila mmoja wetu.
Leo Muhidin Ngurumo (aliyekuwa Msondo Ngoma)  ametangulia.

Pole kwa familia ya Ngurumo, pole kwa wapenzi wote
wa Msondo Ngoma na pole kwa watanzania wote

R.I.P Ngurumo.

Tuesday, April 08, 2014

Watoto Tanzania wanyakua Kombe la Dunia


http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/07/140407084222_tanzania_street_children_team_304x171_bbc_nocredit.jpg
Imebadilishwa: Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro Brazil 06/04/2014.
Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.
Katika mechi ya fainali Tanzania iliibanjua Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3-1 huku mchezaji kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa nyota wa mchezo. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa magoli 2-0. Kipindi cha pili iliongeza bao la tatu. Burundi iliweza kupata bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika nne mpira kumalizika.
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hii ya kombe la dunia.

Hii ilikuwa mara ya Pili kwa timu ya Tanzania kutinga fainali za michuano hiyo ya dunia kwa watoto wa mitaani inayofanyika siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza mwezi Juni. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii kule Durban Afrika Kusini mwaka 2010 Tanzania ilifungwa na India katika fainali. Watanzania tunaweza sana. Mungu awaongoze vijana wetu mzidi fanya vyema zaidi na zaidi.

Mambo nane yakuyajua kuusu wanawake

http://www.baumorthodonticaligners.com/images/start.jpg

Mtu Mmoja mwenye hekima alisema: "Jihadhari na kuwadanganya wanawake kwani wana uhodari wa kujua ukweli na uwezo mkubwa wa kujifanya hawajui". Mwenye kupoteza penzi la mwanamke mwaminifu, amepoteza maisha yake yote.

 
 Je unajua kwamba:-
  1. Mwanamke akiwasiliana nawe sana anamaanisha hataki kuongea na mwingine.
  2. Mwanamke aliyeachwa mara nyingi hupata mwanamme bora kwasababu amejifunza kuchagua kutokana na jeraha lake.
  3. Mwanamke anamiliki hisia sita zaidi ya mwanamme anajua akibadilika au akimsaliti.
  4. Mwanamke anasubiri na kuvumilia sana kuliko mwanamume.
  5. Mara nyingi mwanamke akinung'unika anapendelea kunyamaza.
  6. Mwanamke anaporeact na kukulaumu kwa kosa ambalo wewe ungemtukana, kumpiga au hata kumuacha anamaanisha anakupenda sana.
  7. Mwanamke anapokua amekerwa na mwanamme akanyamaza anatarajia kuwa atabadilika na sio kwa kutojua.
  8. Mwanamke akizungumziwa na mwanamme kuhusu mwanamke mwingine, huficha kilio chake nyuma ya tabasamu lake. 
Kivyo basi usione anacheka unavyowasifia wanawake wengine.
Embu tujuzane wadau kuna ukweli kwenye hili? Mimi naona kama upo vile.