Tuesday, October 29, 2013

Tahadhari juu ya neno MAISHA

 
Elewa sio kila anaye cheka na kufurahi na wewe ukadhani ndie Rafiki,
 Utu wao umo ktk Macho, lakini Nafsi zao zimebeba; Husda, Uadui, Uchawi, Choyo na Roho Mbaya.
 
Furaha zao kukuona unaharibikiwa na hasira zao kukuona umefanikiwa.
 Wangapi uliwaamini, ukawapenda, ukawasaidia, ukawaona ndugu, ukawapa siri zako!
Na LEO ndio maadui zako? Kweli maisha ni watu lakini kuwa muangalifu nao sana!

Credit: Uncle Ngaya.

18 comments:

 1. MMMMH HAPO UMENENA NDUGU

  ReplyDelete
 2. Ujumbe nimeupata wakati muafaka kabisa. Asanteee mpendwa

  ReplyDelete
 3. Replies
  1. kweli kabisa maneno umeyatupa amyna (maneno kuntujeee)

   Delete
  2. Umeona eeeeeh Adam maneno kuntu hasa

   Delete
 4. Yani huu ni bonge la TAHADHALI JUU YA NENO MAISHA.
  keep it up mdada n love u

  ReplyDelete
 5. Tuna kila sababu ya kua waangalifu na hawa watu ambao tunacheka nao na kutuonyesha upendo machoni pasi kujua nafsi zao zina nini juu yetu.

  Ujumbe mzuri sana sana na kama ukiufanyia kazi ujumbe huu ama kwa hakika matatizo ya hapa na pale ya waja yatakupitia mbali kabisa.

  Tuweni makini na hawa marafiki zetu na sio kila rafiki yako wa kumwambia yako ya ndani jamani. Japo kweli maisha ni watu na watu wenyewe ndio hao hao leo marafiki kesho maadui.

  ReplyDelete
 6. Amyna nimependa ulivyo tumia hiyo pic ya mix flower colors. Sababu kila langi ya uwa ina maana yake hapo ukimix na huo ujumbe hapo yani vinaendana sana. Sio kila anaye kuchekea na kukufurahia ana maanisha hivyo na rohoni.

  Keep it up mdada

  ReplyDelete
  Replies
  1. Frank Lymo samahani tumia kiswahili sahihi kidogo.
   Sio UWA ni UA, na SIO LANGI ni RANGI.Samahani kama nitakua nimekukwaza ni vitu vya kawaida tu kuwekana sawa.
   By the way ujumbe ni mzuri.

   Delete
 7. Umeona eeehee

  ReplyDelete
 8. Maneno yana busara sana.

  ReplyDelete
 9. Hao ndio binaadamu wa sasa walivyo furaha zao kukuona unaharibikiwa na hasira zao kukuona umefanikiwa. Mifano hai tunayo cc wenyewe makazini mwetu, majumbani mwetu. Ujumbe ni mzuri

  ReplyDelete
 10. Hawa ndio binaadamu na ndio marafiki zetu
  Ishi nao hivi: Wakikukwepa usijali ipo cku watakutafuta, Wakikusengenya nyamaza huenda watajifunza, Wakikununia omba mungu ipo cku watakuchekea, Wakikuchekea kua makini huenda wanakusanifu Wakikupongeza usiwaamini sana huenda wana kujok, wakikitenga achana nao, wao sio kila kitu kwako, Wakikudhulumu shukuru, mungu atakulipa, Wakikualika mahali kua makini huenda wanakutega.

  Hivyo basi Wakumtumainia na Wakumwamin ni MUNGU pekee na hakuna zaidi yake wala wa kumfananisha nae.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Anony asanteeee yani ni uweli mtupu

   Delete
  2. swadataaaaaaaaa yani hapo umenena anony

   Delete
  3. mmmmmh very very true

   Delete