Mapishi

Asalaam Aleykum wadau wa Amynag Blog Spot.

Katika mwezi huu mtukufu wa ramadhan watu wengi hupenda kufuturu vyakula vizuri nikiwa na maana vilivyo kua na ubora. Kutokana na kuliona hilo nimeona ni vyema wapenzi wangu nikawaletea ukurasa mpya ambao utakua unadeal na mapishi mbali mbali haijalishi ya kiafrika au ya ugaibuni.
Ungana nami AmynaG katika kurasa huu mpya wa mapishi na hata kama wewe mdau una pishi lako na unapenda wanajamii wenzako walijua usisite kuwasiliana nasi...Karibuni tujumuike sote…

Leo napenda tuangalie jinsi ya kupika SAMOSA.

SAMOSA VIPIMO
o Manda ya sambusa
o Mafuta ya kukaangia Kiasi
o Nyama ya Kusaga Kl 1 (au itategemea na kiasi upendacho)
o Kitunguu swaumu kiasi kilicho sagwa
o Tangawizi kiasi kilicho sagwa
o Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
o Pilipili manga 1 kijiko cha supu
o Garam masala 1 kijiko cha supu
o Chumvi Kiasi
o Vitunguu maji vilivyokatwa
o Ndimu moja
o Kotmiri iliyokatwa Kiasi
o Njegere kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
o Weka nyama yako ya kusanga kwenye sufuria lililo safi na uchanganye ndimu, tangawizi, chumvi, pili pili na kitunguu swaumu vyote weka kiasi kwa kulingana na wingi wa nyama alafu bandika jikoni vichemke na kuiva.
o Kabla haija kauka tia Garam masala.
o Chemsha njegere zako na tia chumvi kiasi kidogo sana.
o Vikisha poa vyote kwa pamoja yani nyama na njegere, changanya mchanganyiko wako wa nyama ilio kwisha iva, njegere pamoja na vitunguu maji na kotimiri vilivyo katwa katwa.
o Funga samosa katika manda vizuri au katika mtindo unao penda.
o Pika samosa katika mafuta ya moto hadi ziwe na rangi ya kahawia.
o Ziweke kwenye chombo safi na zitakua tayari kwa kuliwa.
Uzuri wa samosa unaweza kula na soft drinks yoyote soda, juice maziwa ya moto au ya baridi chai au kahawa.
Karibuni Sana na nawapenda wote.

14 comments:

  1. Sambusa Za mboga mboga zinapikwaje?
    naomba tuletee pishi hilo.

    Jane.

    ReplyDelete
  2. Aisee sikua najua kama sambusa za nyama unaweza kuchanganya na njegere. Its good ideal madam

    Sabrina.

    ReplyDelete
  3. Waleykum Msalaam my dia

    uwezi amini nilikua sijui jinsi ya kupika sambusa nilisha zoea kununua tu kwenye vibada, ila sasa nimejifunza kitu kimpya kupitia kwako.

    Asante sana Amyna.

    Mrs Omar

    ReplyDelete
  4. WALEYKUM MSALAAM

    ASANTE KWA PISHI ZURI MOM
    NAOMBA TULETEE PISHI LA MAGIMBI NA NYAMA.

    YUSRA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naku support mdau. Nami nataka kujua hilo pishi la magimbi ya nyama yanapikwaje

      Delete
  5. Waleykum msalaam,

    Amyna naomba kujua jinsi ya kupika kachori na maitaji yake.

    Fatma Issa
    Dom

    ReplyDelete
  6. madam pishi la kababu na kachori plzz. Nitafurahi sana ukituwekea pishi hilo.

    Ms Salama
    DSM

    ReplyDelete
  7. mambo amyna
    naomba kujua pishi la kachori na vitumbua vya shila

    Sakina

    ReplyDelete
  8. Waleykm msalaam amyna
    manda zile za kufungia sambusa zinatengenezwaje?

    Mrs Nassib

    ReplyDelete
  9. manda ya sambusa inatengenezwaje? naomba nielekezwe

    ReplyDelete
  10. mamnda ya sambusa inatengenezwaje?

    ReplyDelete
  11. Maitaji ya utengenezaji wa MANDA YA SAMOSA
    Unga wa ngano nusu ½ kl
    Maji ½ kikombe
    Mafua ya kula kiasi

    Matayarisho:
    Chukua unga wako wa ngano na uweke kwenye chombo kisafi
    Baada ya hapo weka unga wako wa ngano nusu kilo weka maji nusu kikombe
    kanda mchanganyiko wa maji na unga mpaka uwe ngumu ikiwa laini itakusumbua na itakatika katika
    Sukuma mduara mdogo kisha paka mafuta ya kula juu yake
    Mwagia unga kiasi kuzunguka mduara wote kusaidia manda zisishikane baada ya kuchomwa
    Kusukuma kisha paka mafuta halafu nyunyizia unga kisha zipandanishe kwa juu mpaka zifike
    Miduara kati ya mitano au saba itategemea na nguvu yako ya kusukuma. Ukiweka manda tano zitatoa samosa ishirini na ukiweka manda saba zitatoa zitatoa manda samosa ishirini na nane
    Kisha usukume mduara huo wenye samosa tano au saba mpaka upate chapati moja nene na pana usawa wa kikaangio chako
    Choma katika kikaango kwa moto wa wastani ili usiunguze choma dakika mbili hadi tatu kila upande kisha geuza
    baada ya hapo toa ikiwa ya moto anza kuzibandua kwa haraka kabla hazijapoa
    Kata kati kwa kati pande nne kwa usawa
    Kata kuzunguka manda hiyo ili kuweka mzunguko sawa
    Chukua unga kiasi na maji changanya iwe nzito itatumika kama gundi
    Kunja manda yako uliyo kata upande wa kulia hakikisha unaandamiza ili gundi ikamate
    Kunja upande wa kushoto kandamiza pia ili gundi ishike
    Baada ya hapo upannde wa chini utakuwa wazi ni kwa ajiri ya kujaza nyama kama samosa ya nyama au mbonga mboga kama samosa ya mboga mboga
    Chukua kijiko kisha weka nyama katika manda yako au mboga mboga katika manda yako
    utamalizia kwa kupaka gundi ule upande ulio baki baada ya kujaza nyama zako paka gundi kwa juu kisha funga manda yako.

    Huo ndio utengenezaji wa manda ya samosa. Nafikiri umenielewa Devotha Majula na karibu.

    ReplyDelete
  12. Hi Amyna, nimetafuta kujua saana jinsi ya kutengeneza Manda, hapa leo nimepata , Nashukuru sana.Ila bado sijakupata vizuri Pale uliposema ''ukishasukuma kwa mduara wako, weka kwenye kikaango cha moto,alafu tena kuzibandua, ''Sielewi, si zitakua ngumu tayari,, na je unaweka zote kwa mpigo??? AHSANTE

    ReplyDelete
  13. Dear Anony June 27, 2014 at 12:36

    Naomba pitia tena haya maelezo kwa udhuli kabisa jibu lako nipo hapa mpendwa.

    "Sukuma mduara mdogo kisha paka mafuta ya kula juu yake,Mwagia unga kiasi kuzunguka mduara wote kusaidia manda zisishikane baada ya kuchomwa. Kusukuma kisha paka mafuta halafu nyunyizia unga kisha zipandanishe kwa juu mpaka zifike miduara kati ya mitano au saba itategemea na nguvu yako ya kusukuma. Ukiweka manda tano zitatoa samosa ishirini na ukiweka manda saba zitatoa zitatoa manda samosa ishirini na nane. Kisha usukume mduara huo wenye samosa tano au saba mpaka upate chapati moja nene na pana usawa wa kikaangio chako".

    Ahsante na twashukuru kwa kutembelea blog yetu.

    ReplyDelete