Tuesday, February 12, 2013

Tujuzane

Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako
 
Herufi A
Mwenye jina linaloanziana na herufi a ni mtu anayependa mambo makubwa,
anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake.
Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda kuheshimiwa, anapenda
Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha nyota ya punda.
 
Herufi B
Mwenye jina linaloanziana na herufi b ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi.
Ni jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
Herufi B inawakilisha nyota ya ngombe.
 
 
Herufi C
Mwenye jina linaloanziana na herufi c ni mtu wa kukubadilika
Badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa
Wabunifu na wanaopenda mawasiliano herufi C inawakilisha nyota ya mapacha.
 
Herufi D
Mwenye jina linaloanziana na herufi d ni mtu anayependa usawa, biashara.
Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi.
Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi D inawakilisha nyota ya kaa.
 
Herufi E
Mwenye jina linaloanzia na herufi e ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma.
Mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni
Mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E inawakilisha nyota ya simba.
 
Herufi F
Mwenye jina linaloanzia na herufi f ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na
Ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa
Kufanya maamuzi. Herufi F inawakilisha nyota ya mashuke.
 
Herufi G
Mwenye jina linaloanzia na herufi g ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho.
Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni mtu mwenye hisia kali, msomi, mpweke
Na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G inawakilisha nyota ya mizani.
 
Herufi H
Mwenye jina linaloanzia na herufi h ni mtu mwenye ubunifu
Na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake.
Ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. Herufi H inawakilisha nyota ya nge.
 
Herufi I
Mwenye jina linaloanzia na herufi i ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu.
Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
Herufi I inawakilisha nyota ya mshale.
 
Herufi J
Mwenye jina linaloanzia na herufi j ni mtu mwenye
Matamanio, mkweli, mkarimu na muerevu. Asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa.
Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J inawakilisha nyota ya mbuzi.
 
Herufi K
Mwenye jina linaloanzia na herufi k ni mtu mwenye jeuri.
Mwenye msimamo thabiti, mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na
Kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. Ni mtu
Asioridhika na hali ya kimaisha. Herufi K inawakilisha nyota ya ndoo.
 
Herufi L
Mwenye jina linaloanzia na herufi l ni mtu wa vitendo,
Mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata
Ajali mara kwa mara. Herufi L inawakilisha nyota ya samaki.
 
Herufi M
Mwenye jina linaloanzia na herufi m ni mtu mwenye kujiamini sana,
Mchapakazi na hupata mafanikio. Ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
Herufi M inawakilisha nyota ya punda.
 
Herufi N
Mwenye jina linaloanzia na herufi n ni mtu mwenye ubunifu,
Hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
Herufi N inawakilisha nyota ya ngombe.
 
Herufi O
Mwenye jina linaloanzia na herufi o ni mtu mwenye subra,
Mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda
Kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
Herufi O inawakilisha nyota ya mapacha.
 
Herufi P
Mwenye jina linaloanzia na herufi p ni mtu mwenye uwezo
Wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini
Anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi P inawakilisha nyota ya kaa
 
Herufi Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili.
Ni watu wasiyoelezeka na wana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu
Aliyepooza sana. Herufi Q inawakilisha nyota ya simba.
 
Herufi R
Mwenye jina linaloanzia na herufi r ni mtu mwenye uvumilivu,
wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
Herufi R inawakilisha nyota ya mashuke.
 
Herufi S
Mwenye jina linaloanzia na herufi s ni mtu mwenye mvuto
Mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
Herufi S inawakilisha nyota ya mizani 
 
Herufi T
Mwenye jina linaloanzia na herufi t ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia
Nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda
Mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi T inawakilisha nyota ya nge.
 
Herufi U
Mwenye jina linaloanzia na herufi u ni mtu mwenye bahati
Kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na
Aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha nyota ya mshale.
 
Herufi V
Mwenye jina linaloanzia na herufi v ni mtu mchapakazi,
Wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.
Herufi V inawakilisha nyota ya mbuzi. 
 
Herufi W
Mwenye jina linaloanzia na herufi w ni mtu muwazi,
Wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya.
Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha nyota ya ndoo.
 
Herufi X
Mwenye jina linaloanzia na herufi x ni mtu asiyependa
Kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.
Herufi X inawakilisha nyota ya samaki.
 
Herufi Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi y ni mtu mwenye kupenda uhuru na hawapendi kupingwa
Jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati
Katika maisha. Herufi Y inawakilisha nyota ya punda.
 
Herufi Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani.
Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.
Herufi Z inawakilisha nyota ya ngombe.
 
Tx Mr Isaac Katembo
Lov u ol…..xoxoo

No comments:

Post a Comment