Monday, July 22, 2013

Chapati

Wadau Asalaam Aleykum kwa Waislam wote na Bwana Asifiwe kwa Wakristu wote.
Leo dada yenu naja na pishi la CHAPATI. Najua ni kitafundwa pendwa sana na kinapendwa na kila lika.
Uzuri wake chapati bwana unaweza kulia na chochote kile, iwe maharage, supu aina zote, mchuzi uwe wa kuku, wa samaki, wa nyama yani raha tupu hapa hata na chai inapanda kwa soda na juice tena ndio balaaa.
Kwa kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadan chapati hua zinalika hasa tena sana sana hua zinaambatana na mchuzi no matter wa kitoweleo gani.
Tuungane pamoja katika safu yetu na tushare pamoja mawazo yetu.
 
 
Mahitaji
ü  Unga wa ngano (Plain flour 1kilo)
ü  Siagi (Butter vijiko 2 vya chakula)
ü  Yai (Egg 1)
ü  Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
ü  Hiliki (Ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
ü  Maji ya uvuguvugu (Warm water)
ü  Mafuta ya kupikia (Vegetable oil)
 
Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na  hiliki iliyo twangwa na uchanganye kwanza mpaka mchanganyiko wako uchanganyike.
Tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri.
Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge.

Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe laini.
ambapo itakuchukua kama dakika kumi au kumi na tano hivi. Baada ya hapo kata kata unga wako katika madonge ya wastani yani si makubwa si madogo.
Baada ya hapo andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao.
Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze.
Ukisha maliza ikunje (roll). Ufanye hivyo na kwa madonge yote yalio bakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani.
Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika).
Ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea.
Acha iive upande mmoja kwanza alafu uigeuze na  upande wa pili.
Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha.
Utaendelea kufanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyo hiyvo mpaka chapati iive.
Utaitoa na kuiweka kwenye sahani na itakua tayari kwa kuliwa.

Utafanya hivyo kwa madonge yako ya chapati yote yaliyo bakia.

Swaum Njema na Ramadan Kareem.

2 comments:

  1. Mmmmh Ma Sha Allah. Mamii nilikua cjui kama kwenye chapati waweza tia siagi. Nimefata hayo maelezo yako chapati zimetoa nzuri na tamu hatari.

    Asante sana Amyna na ubarikiwe

    ReplyDelete
  2. haya mama maanjumati hayo...lol

    ReplyDelete