Tuesday, October 27, 2015

Uchaguzi Mkuu Tanzania Oktoba 25, 2015.

Uchaguzi Mkuu Tanzania Oktoba 25, 2015.
 
Namuomba sana Mungu wangu (Allah) Uchaguzi upite salama bila ya machafuko ya aina yoyote na wagombea wote napenda wakumbuke kua Siasa sio ajila na cheo ni dhamana, sasa haya mambo ya kuto kukubali matokeo kama upemeshidwa ndio nini?? ama tukueleweje?? Kuna msema wa wahenga walisema “asie kubali kushindwa sio mshindani”.
 
Yote kwa yote watanzania wenzangu tusikubali kushawishika kuvuruga amani yetu maana amani ikipotea ni ngumu sana kurudi tena, embu tuone Inchi za wenzetu watu wanavyoangaika, mauwaji ya kila uchao, watu hawali wakashiba, hawafanyi maendeleo ya aina yoyote kutwa kucha ni kukimbia tu. Jamani tulindeni amani yetu kwani ni hadhina kubwa sana sana.
 
Binafsi mimi sipo upande wa chama chochote na nimechagua Raisi, Mbunge na Diwani kutokana na sera zao, utendaji kazi wao n.k sijachangua kwa kufuata mkumbo wa mtu.
 
Watanzania tuache tabia ya kujitolea matokeo wenyewe maana kila mtu anatoa matokeo yake utazani yeye ndio msemaji wa tume matokeo yake watu wanakinzana huko mitaani na mitandaoni, tushaambiwa tutulie tume inafanya kazi yake na tume ndio chombo pekee kinakachotoa matokeo ya walio pita kwenye uchaguzi.
 
Mungu(Allah) wabariki washindi wote ambao mpaka sasa wameshatangwazwa na tume na wanaoendelea kutangazwa na tume, Ya Allah uwajaze busara, imani, upendo miyooni mwao waweze kulitumikia Taifa hili kwa mioyo yao yote bila ya kufanya matendo ya kifisadi, watimize ahadi zao walito zisema kwa wanainchi wao, washirikiane na wanainchi katika kuleta maendeleo ya maeneo yao na Taifa kwa ujumla, Ukawajaze busara na uwape muongozo ulio tukuka katika kufanya maamuzi yoyote yanayo usu masaili ya Taifa hili...wote tusema Ameeeen.
 
Tudumisheni Amani, Upendo na Mshikamano.
Naipenda Tanzania yangu, Nawapenda Watanzania wenzangu wote.
Mungu ibariki Tanzania na Mungu tubariki Watanzania wote.

No comments:

Post a Comment