Monday, August 06, 2012

Vitumbua

Vitumbua ni vitafunwa pendwa vinavyo pendwa na watu wote.
Jinsi ya kuanzaa na kuvipika.

Mahitaji:
o   Unga wa mchele 1 kg
o   Sukari nusu kikombe cha chai
o   Tui bubu la nazi la kutosha kuchanganyia unga wako
o   Mayai mawili
o   Mafuta ya kupikia
o   Unga wa hiliki nusu kijiko cha chai
o   Hamira kijiko 1 cha chai
o   Unga wa ngano vijiko viwili vya chakula
o   Chuma cha kuchomea vitumbua

Namna ya kuandaa na kupika:
o   Chukua bakuli kubwa kiasi ambalo litatoshea mchanganyiko wako akikisha bakuli lako safi
o   Chukua unga wako wa mchele uweka ndani ya bakuli na unga wako wa ngano pia tia ndani ya bakuli hilo
o   Tia hamira, sukari changanya mchanganyiko huo kwanza mpaka uchanganyike vizuri
o   Vyunja yai lako tia ndani ya bakuli ambalo lina mchanganyiko wako, weka na tui bubu lako kisha changanya  mchanganyiko wako vizuri mpaka uwe laini bila ya mabuja buja
o   Chukua unga wako wa hiliki na uweke kwenye mchanganyiko wako baada ya hapo endelea kuchanganya mpaka uakikishe mchanganyiko wako umechanganyika vizuri
o   Akikisha mchanganyiko wako sio mwepesi au mzito sana uwe wa wastani
o   Acha uji wako huo kwa  dakika 45 au saa 1 ili uumuke
o   Hatua ya mwisho washa jiko lako na chukua chuma chako cha kuchomea vitumbua akikisha ni kisafi kiweke kwenye jiko na hakikisha kimepata moto
o   weka mafuta kijiko kimoja cha chakula katika kila kichumba cha chuma chako cha kuchomea vitumbua yakipata   moto anza kuweka uji wako ili uchome vitumbua
o   Akikisha vimeiva vizuri na vimekua na rangi nzuri vitoee na vipange kwenye sahani na vitakua tayari kwa kuliwa.

 Swaum njema n nawapenda wote….Xoxoo

3 comments:

 1. mmmmmh ctaki kujua utamu wa hivi vitumbua... so nice

  Mrs Nassib

  ReplyDelete
 2. Kumbe vitumbua unaweza changanya na mayai,,, sikua nalijua hilo my dear asante sana na ubalikiwe

  Lilian

  ReplyDelete
 3. Daah!! wewe ni noma wangu.

  Julias

  ReplyDelete