Friday, July 11, 2014

Mapishi ya Kebabu

Haya jongeeni kijiweni tuongezeane ujuzi wa mapishi. Angalia upishi wa KEBABU.
Mahitaji
 1. Nyama ya kusaga kl 1
 2. Kotmili/giligilani wengine huita kifungu kimoja
 3. Kitunguu maji vikubwa vitatu
 4. Swaum kikubwa kimoja & tangawizi
 5. Mikate ile ya elfu moja nunua miwili ama mitatu
 6. Chumvi kiasi
 7. Binzali nyembamba na pilipili manga vilivyo sagwa
 8. Pili pili hoho kubwa moja
 9. Mafuta ya kupikia
 10. Ndimu
 11. Mayai sita
Hatua ya kwanza
Nyama ya kababu hua aichemshwi habisa. Kumbuka nyama kama ina maji yakamua. Chukua nyama yako weka kwenye chombo kisafi, tia chumvi, ndimu, unga wa binzari nyembamba, kamulia na ndimu kisha tia pilipili manga, alafu changanya huo mchanganyiko wako na uakikiche umechanganyika vizuri kabisa.
Hatua ya pili
Katakata vitunguu maji katika vipande vidogo vidogo kama vya sambusa vile, katakata pia pili pili hoho zako katika mfumo huo huo pamoja na karoti, osha kotmili/giligilani zako vizuri na ukamue maji alafu toa ile mizizi ya nyuma na kisha katakata katika vipande vidogo vidogo, twanga swaum zako pamoja na tangawizi na badala ya hapo tia katika mchanganyiko wako ule wa nyama. Changanya mpaka uakikiche umechanganyika vizuri. Kuonja ruksa wapenzi iliuweze jua kama vitu vyote vipo sawa au laa....
Hatua ya tatu
Chukua mikate yako toa ile nyama ya kati nikimaanisha ile nyama ya mkate nyeupe ule upindo wa pembeni usiweke sababu ni mgumu na sio soft. Chambua mikate yako vizuri kabisa na inyambue nyambue na uweke katika mchanganyiko wako wa nyama, chukua mayai matatu uweke humo. Changanya vyote sasa kwa pamoja mpaka uwakikiche vimechanganyika ipasavyo. Na baada ya hapo utafanya kama unakanda unga wa ngano vilee na upate donge moja takatifu. Utaacha mchanganyiko wako kwa mda wa kama dk 10 or 15 hivi ili viungo viweze kukolea kwa uzuri.
Hatua ya nne na mwisho
Kata vidonge vidodo vidogo ama upendavyo na kutengeneza style uipendayo, weka kwenye chombo safi, vyunja mayainyako yale matatu yalio baki na uweke kwenye bakuli toa vile viini vya ndani na ubaki na ute tu. Weka kikaangio chako jikoni na usiwe na moto mkali, moto uwe wa wastani tu, mafuta yako yakisha pata moto chukua kebabu zako tosa kwenye ule ute wa yai na uweke kwenye mafuta yakio jikoni na utarudia kwa vyote viduara ulivyo fanya. Baada ya hapo vitakua tayari kwa kuliwa. Ni tamuje sasa.....Very yummy waweza sukumia na chochote Wallah.

Cha ziada
Wapenzi alafu ule mkate ulio utoa ule mgumu (upindo wa mkate) hautupwi wapendwa. Unaufanya hivi; Ukaushe kwenye microwave ukauke vizuri usiungue. Alafu utwange huo mkate wako mpaka upate unga unga. Baada ya kukata madonge yako ya kebabu unaweka kwenye huo unga viliga viliga ukitoa unaweka kwenye ute wa yai utafanya hivyo mara mbili na kasha utachoma.









Amynag tunawapenda sana 
Ramadan Makbul & Ijumaa Kareem.
Enjoy


1 comment:

  1. By God yesterday nimejalibu pika KEBABU jamani jamani tamuje sasa.
    Uwiiii barikiwa mama uendeleee kutuletea vizuri vingine

    ReplyDelete