Tuesday, June 19, 2012

Unabishaa!!!!


Ninakuhakikishia katika sifa hizi kumi lazima wewe ulikuwa nazo kadhaa.

1. Ulishacheza kibaba babaa/ kimama mama.
2. Ulikuwa mwizi wa sukari.
3. Wakati wa sikukuu usiponunuliwa nguo mpya unalia.
4. Ulishadanganya unaumwa ili tu, usiende shule.
5. Ulishapangusa kamasi kwa shati la shule au mkononi (pakuvalia saa).
6. Ulishawahi kulia kisa umelazimishwa kuoga.
7. Ulishanawa mikono, miguu, uso na kichwa kisa unaogopa baridi na kujidai umeoga.
8. Ulishawahi kudokoa mboga jikoni.
9. Ulicheza kombolela, makida makida, malede, kipande, mdako, kucheza vichupa na vitambaa pamoja na kifimbo cheza..

10. Ulikuwa kikojozzzzzzzzz

Unalo la kubisha……..!!! Nimekugusa kunako hahahahahaa hapana chazea utoto.

Asante sana kaka Kusekwa Machibya.
Nawapenda wote..Xoxo

6 comments:

 1. Hahahahaa Kweli umegusa kunako dada.

  Kajuna

  ReplyDelete
 2. Aiseee mie hiyo #3 yani inanihusu kabisa uwiii.

  Mrs Nassib

  ReplyDelete
 3. Hahahaahah hakuna kuisha kabisa yani ni ukweli mtupu wangu...kweli hapana chezea utoto.

  Frank

  ReplyDelete
 4. Atakae bisha huyo muongo wa mwaka. Teheehe tehh umenikumbusha mbali sana Amyna mie hiyo namba nne yani nimeifanya sana walai looh! mwenyewe nilikua najua nakomoa wazazi wangu kumbe nilikua najikosesha kujua vitu muhimu.

  Utoto kweli sio kabisa
  Juliana

  ReplyDelete
 5. Kweli kabisa Juliana atakae bisha uyo ni muongo wa mwaka. Hakuna mtoto ambae hajapitia kimoja ama nusu ya haya au yote haya.

  Lengo la kupost hii kitu ni kutaka kuwafurahisha na kuwakumbusha mambo tulio ya fanya tukiwa watoto.

  Hahahahah utoto raha jamani.
  Thnks n Love u all.

  ReplyDelete
 6. umenikumbusha nbali sana amyna
  enzi hizo ucpo nunuliwa nguo ya sikukuu mbona home akukaliki, mambo ya kudokoa sukari ndio ucseme.

  Keep it up Amyna

  ReplyDelete