Saturday, May 04, 2013

MATOKEO KIDATO CHA NNE KUPANGWA UPYA


  Mdau umeisikia hili toka baraza la mitihani
 
Serikali imetangaza uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato cha nne ya 2012. Uamuzi huo umetangazwa mapema leo bungeni na Waziri William Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu iliyokuwa inachunguza kuhusu matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa kwa utaratibu tofauti na uliokuwa unatumika zamani.

Tetesi za awali zilieleza kwamba matokeo hayo yalipangwa kwa kuzingatia madaraja haya hapa chini, japo Baraza la Mitihani lilikanusha baadaye kwa kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli.

A = 80%-100%-
 B = 65%-79%-
 C = 50%-64%-
 D = 35%-49%-
 F = 0%-34%-

Tume ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa madaraja tofauti na uataratibu wa awali. Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa hayatatumika tena mpaka yaje yaliyopangwa upya. HakiElimu itatoa taarifa rasmi baadaye kuhusu uamuzi huu wa serikali.


Kila la kheri.

No comments:

Post a Comment