Tuesday, April 29, 2014

Utaratibu wa lishe maalum kwa wanaopenda kupunguza uzito




Habari za wakati huu wapendwa wangu.
Embu tuunganeni tena katika diet hii. Hichi kitu nimetumiwa leo asubuhi na kipenzi changu, shoga yangu, roho yangu bibie JULLY BHERA. Ahsante sana kipenzi Jully Bhera kwa kunipatia diet hii. Penda sana wewe Wallah.

 Huu ni utaratibu wa kula kwa mpangilio ambapo nidhamu ya hali ya juu inahitajika ili kufikia lengo ulilo kusudia. Nidhamu ni kitu muhimu sana si kwa diet tu hata katika mambo mengine ili uweze fikia malengo uliyo jiwekea.

Ukifanikiwa kufuata maelekezo haya una uwezo wa kupunguza kati ya kilo 10 – 15 katika kipindi cha wiki mbili mfululizo kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Zingatia wakati wote wa diet usinywe soda wala bia, usile peremende (pipi) wala big g bali kunywa maji kwa wingi sana. Diet hii hufanywa kwa wiki mbili mfululizo kisha unapumzika na kurudia tena baada ya miezi mitatu.

Jumatatu
Asubuhi: Kikombe cha kahawa na sukari kidogo.
Mchana: Kipande kidogo cha nyama nyembamba iliyochemshwa na nyanya moja.
Usiku: Nyama steki robo kilo iliyochemshwa, kachumbali ya kijani iliyotiwa chumvi kidogo pamoja na limao au ndimu na hakikisha unakunywa maji kwa wingi.
 
Jumanne
Asubuhi: Kikombe cha kahawa na sukari kidogo.
Mchana: Kipande kidogo cha nyama nyembamba iliyochemshwa au soseji mbili.
Usiku: Nyama kiasi iliyochemshwa au mishikaki isiyo na mafuta na kachumbali ya kijani yenye ndimu au limao na maji kwa wingi.
 
Jumatano
Asubuhi: Kikombe kidogo cha kahawa na sukari kwa mbali na slesi moja ya mkate iliyochomwa.
Mchana: Mayai mawili na kipande cha nyama nyembamba ya kuchomwa au soseji tatu na kachumbali ya kijani na ndimu au limao.
Usiku: Mboga mbali mbali za majani zilizo chemshwa kama mchicha, karoti na nyanya moja, kula tunda moja lisolo na sukari nyingi na maji kwa wingi.
 
Alhamisi
Asubuhi: Kikombe cha kahawa na sukari kidogo.
Mchana: Glasi moja ya maziwa mtindi au glasi moja ya juisi isiyoungwa na sukari (namaanisha juisi fresh sio za mabox au za kununua vibandani)
Usiku: Yai moja la kuchemshwa, karoti tatu za kuchemshwa na jibini au chizi na maji kwa wingi.
 
Ijumaa
Asubuhi: Karoti tatu zilizosagwa na kutiwa ndimu ndio kiwe kifungua kinywa chako.
Mchana: Samaki mmoja mkubwa aliyechemshwa na siagi kidogo.
Jioni: Robo kilo ya nyama steki isiyo na mafuta iliyochemshwa pamoja na kachumbali ya kijani na ndimu ama limao, kula na mboga za majani uzipendazo kama karoti, pilipili hoho na kumbuka kunywa maji kwa wingi hasa.
 
Jumamosi
Asubuhi: Kahawa kikombe kimoja sukari kwa mbali na slesi moja ya mkate iliyochomwa.
Mchana: Mayai mawili saga na karoti tatu weka na ndimu ama limao iwe ndio kichwaji chako kwa huo mlo wako wa mchana.
Usiku: Nusu kuku wa kienyeji awe kokoo au jogoo ila asiwe na mafuta mchemshe au mchome waweza sukumizia na kachumbali ya kijani iliyo na ndimu ama limao. Maji ndio kila kitu hivyo basi akikisha unakunywa maji kwa wingi.
 
Jumapili
Asubuhi: Chai ya rangi kikombe kidogo weka na sukari kidogo.
Mchana: Hakuna kula kitu.
Usiku: Huu ni usiku wa mwisho wa diet yako, kula nyama iliyo chomwa nusu kilo, kula matunda mengi uwezavyo.

Ujumbe wangu kwenu
 Utafanya hivyo hivyo kwa wiki ya pili pia, kwa hakika ukifuata mpangilio huu utafanikiwa, kama una matatizo ya kiafya ni vyema ukapata ushauri wa Daktari kwanza kabla ya kuanza kufanya diet. Sio kwa diet hii hata kwa diet yoyote ile. Napenda kukusisitizia unywaji wa maji mengi ni muhimu sana katika uimalishaji wa afya zetu na jijengee tabia ya kunywa maji walau liter mbili ama mbili na nusu kwa siku.
 





No comments:

Post a Comment