Adhabu ya kiboko kwa wanafunzi
imeharamishwa katika shule zote nchini Kenya
Wazazi katika
kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu
kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.
Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na
mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.
Wazazi hao waliandamana kwa amani wakitaka
hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Hata hivyo polisi waliweza kumkamata
mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.
Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba
katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.
Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu
kumchapa kwenye kisogo.
Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia kile
wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo walitaka
mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo hicho cha kumchapa mwanafunzi
ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini Kenya.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika
shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine.
Kenya
iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi
iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na
kuwajeruhi kukithiri.
Kwa msaada wa BBCSwahili.com
No comments:
Post a Comment