Idhaa ya BBC
kitengo cha Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya
virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizonaswa kisiri
zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata
vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo
visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri
kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine
Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila ya kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo
zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hawana virusi
vinavyosababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo
kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika
maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda, Kampala
zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
BBC ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana
Rugunda, ushahidi huo, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini
akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashitaki
wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa
cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi
wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuwa
Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia.
Kwa
msaada wa BBCSwahili.com
Mmmh majanga
ReplyDelete