Serikali ya Afrika Kusini imeanza mpango wa kuwapa vijana
wa shule za sekondari kuendelea juu mipira ya Condom zenye rangi tofauti
tofauti na ambazo zina harufu nzuri ya kuvutia.
Mpango huu unalenga kuzuia wanafunzi kuchoka kutumia
mipira ya kawaida ya condom wanaposhiriki ngono.
Waziri wa afya Aaron Motsoaledi, ameyasema hayo baada ya
utafiti uliofanywa nchini humo kuonyesha kuwa matumizi ya mipira ya Condom
imepungua nchini Afrika Kusini.
Inaarifiwa kinachosababisha upungufu huo ni kwamba Condom
za kawaida zinazotolewa na serikali hazina mvuto wowote kwa vijana.
Afrika Kusini ina watu milioni 6.4 wanaoishi na virusi
vya HIV, idadi hiyo ikiwa juu zaidi kuliko nchi yoyote duniani.
Utafiti uliofanywa na kitengo cha serikali cha utafiti wa
afya, ulionyesha maambukizi yameongezeka hadi asilimia 12.2.
Takriban watu milioni 2 hupata matibabu ya ARV's au
madawa ya kupunguza makali ya HIV.
Hata hivyo baadhi ya mashirika ya misadaa yanaonya kuwa
baadhi ya kliniki zinakabiliwa na upungufu wa dawa hizo.
Condom hizo zitatolewa na serikali kwa vijana bila
malipo.
Kwa msaada wa BBCSwahili.com
No comments:
Post a Comment