Mahitaji
Kumbuka:
kuanza maandalizi
mapema ili tui ligande kwenye mbaazi zako.
ü Mbaazi mbichi au
Mbaazi kavu - ½ kl
ü Kitunguu maji - Kikubwa
kimoja 1
ü Kitunguu swaum – Kiasi
cha punje nne/tano
ü Karoti – Moja kubwa
ü Pili pili hoho – Moja
kubwa
ü Chumvi - Kiasi
ü Manjano - ½ Kijiko
cha chai
ü Mafuta ya kupikia (Vegetable
oil) – Kijiko kimoja cha chai
ü Pilipili mbichi – Moja
moja nzima
ü Nazi (Coconut nature)
– Tatu kubwa
ü Giligilan
ü Unga
wa ngano (Plain flour)
– kijiko kimoja cha chakula
Matayarisho na kupika
Hatua ya kwanza:
ü Osha mbaazi kwenye
chungio na ziache zitoke maji.
ü Chambua kitunguu maji
chako, kisafishe na ukikate vipande vidogo vidogo katika shape nzuri .
ü Chambua kitunguu
swaum vyako vitwange mpaka vilainike vizuri.
ü Osha karoti na pili
pili hoho kisha uvikate vidogo vidogo katika shape nzuri
ü Kuna nazi (coconut
nature) yako vizuri iwe laini na uichuje matui mawili, tui bubu(tui la kwanza)
na tui la pili.
Kupika kwa mbaazi mbichi
ü Chemsha mbaazi zako
mbichi kwa maji hadi ziive lakini zisirojeke ziwe ngumu kidogo.
ü Chukua tui lako la
weka kwenye mbaazi zako pamoja na mchanganyiko wa karoti na nk.
ü Weka tena jikoni
vichemke na mpaka tui lako likauke kabisa.
ü Mimina mbaazi zako
kwenye trei ili zipoe na ni vyema zikapoa kabisa ili tui lako ukija kumwagia
juu lisiyeyuke.
ü Chukua tui lako bubu
weka jikoni, weka kijiko cha chakula plat unga wa ngano
(Plain flour).
ü Koroga
bila ya kuacha hadi tui lako lichemke, kisha koroga manjano yako kwenye kikombe
weka kiasi.
ü Changanya
kwenye tui lako unalo lipika akikisha tui lako lina kua zito zito.
ü Ipua
na pooza kodogo tui lako.
ü Mwagia
juu ya mbaazi ukiwa unasambaza kama icesugar kwenye cake.
Kupika kwa mbaazi kavu
ü Chambua mbaazi na
kutoa uchafu osha na loweka mbaai zako usiku kucha.
ü Mbaazi zina tabia ya
kunyonya maji hivyo basi weka kwenye kikubwa na ujaze maji
ü Asubuhi zitoe kwenye
maji na ubadike jikoni weka maji hadi zitakapo anza kuiva
ü Punguza moto ili
ziive kwa moto mdogo ili zisi pasuke.
ü Chuja nazi na tui
bubu weka pembeni tumia lile tui la pili.
ü Hilo tui la pili weka
kwenye mbaazi zako pamoja na mchanganyiko wako wa vitunguu maji, hoho na nk.
ü Weka tena jikoni ili
hilo tui la pili na mchanganyiko wako uchanganyike na tui lako liivi na
likauke.
ü Ipua na umimine
kwenye trei wacha zipoe.
ü Chukua tui lako bubu
weka jikoni, weka kijiko cha chakula plat unga wa ngano
(Plain flour).
ü Koroga
bila ya kuacha hadi tui lako lichemke, kisha koroga manjano yako kwenye kikombe
weka kiasi.
ü Changanya
kwenye tui lako unalo lipika akikisha tui lako lina kua zito zito.
ü Ipua
na pooza kodogo tui lako.
ü Mwagia
juu ya mbaazi ukiwa unasambaza kama icesugar kwenye cake.
ü Na baada aya hapo mbaazi
zako zitakua tayari kwa kuliwa
Kumbuka:
Unaweza kulia na
chochote kile, iwe chapati, wali, maamri (maandazi),vitumbua yani raha
tupu.
Pishi:
Limetetwa kwenu na bidada Sware Kaku. Asante sana mama naenda fanyia kazi hii
kitu.
Ramadan kareem
na siku njema kwetu sote In Sha Allaah.