Mahitaji
Kumbuka:
kuanza maandalizi
mapema ili tui ligande kwenye mbaazi zako.
ü Mbaazi mbichi au
Mbaazi kavu - ½ kl
ü Kitunguu maji - Kikubwa
kimoja 1
ü Kitunguu swaum – Kiasi
cha punje nne/tano
ü Karoti – Moja kubwa
ü Pili pili hoho – Moja
kubwa
ü Chumvi - Kiasi
ü Manjano - ½ Kijiko
cha chai
ü Mafuta ya kupikia (Vegetable
oil) – Kijiko kimoja cha chai
ü Pilipili mbichi – Moja
moja nzima
ü Nazi (Coconut nature)
– Tatu kubwa
ü Giligilan
ü Unga
wa ngano (Plain flour)
– kijiko kimoja cha chakula
Matayarisho na kupika
Hatua ya kwanza:
ü Osha mbaazi kwenye
chungio na ziache zitoke maji.
ü Chambua kitunguu maji
chako, kisafishe na ukikate vipande vidogo vidogo katika shape nzuri .
ü Chambua kitunguu
swaum vyako vitwange mpaka vilainike vizuri.
ü Osha karoti na pili
pili hoho kisha uvikate vidogo vidogo katika shape nzuri
ü Kuna nazi (coconut
nature) yako vizuri iwe laini na uichuje matui mawili, tui bubu(tui la kwanza)
na tui la pili.
Kupika kwa mbaazi mbichi
ü Chemsha mbaazi zako
mbichi kwa maji hadi ziive lakini zisirojeke ziwe ngumu kidogo.
ü Chukua tui lako la
weka kwenye mbaazi zako pamoja na mchanganyiko wa karoti na nk.
ü Weka tena jikoni
vichemke na mpaka tui lako likauke kabisa.
ü Mimina mbaazi zako
kwenye trei ili zipoe na ni vyema zikapoa kabisa ili tui lako ukija kumwagia
juu lisiyeyuke.
ü Chukua tui lako bubu
weka jikoni, weka kijiko cha chakula plat unga wa ngano
(Plain flour).
ü Koroga
bila ya kuacha hadi tui lako lichemke, kisha koroga manjano yako kwenye kikombe
weka kiasi.
ü Changanya
kwenye tui lako unalo lipika akikisha tui lako lina kua zito zito.
ü Ipua
na pooza kodogo tui lako.
ü Mwagia
juu ya mbaazi ukiwa unasambaza kama icesugar kwenye cake.
Kupika kwa mbaazi kavu
ü Chambua mbaazi na
kutoa uchafu osha na loweka mbaai zako usiku kucha.
ü Mbaazi zina tabia ya
kunyonya maji hivyo basi weka kwenye kikubwa na ujaze maji
ü Asubuhi zitoe kwenye
maji na ubadike jikoni weka maji hadi zitakapo anza kuiva
ü Punguza moto ili
ziive kwa moto mdogo ili zisi pasuke.
ü Chuja nazi na tui
bubu weka pembeni tumia lile tui la pili.
ü Hilo tui la pili weka
kwenye mbaazi zako pamoja na mchanganyiko wako wa vitunguu maji, hoho na nk.
ü Weka tena jikoni ili
hilo tui la pili na mchanganyiko wako uchanganyike na tui lako liivi na
likauke.
ü Ipua na umimine
kwenye trei wacha zipoe.
ü Chukua tui lako bubu
weka jikoni, weka kijiko cha chakula plat unga wa ngano
(Plain flour).
ü Koroga
bila ya kuacha hadi tui lako lichemke, kisha koroga manjano yako kwenye kikombe
weka kiasi.
ü Changanya
kwenye tui lako unalo lipika akikisha tui lako lina kua zito zito.
ü Ipua
na pooza kodogo tui lako.
ü Mwagia
juu ya mbaazi ukiwa unasambaza kama icesugar kwenye cake.
ü Na baada aya hapo mbaazi
zako zitakua tayari kwa kuliwa
Kumbuka:
Unaweza kulia na
chochote kile, iwe chapati, wali, maamri (maandazi),vitumbua yani raha
tupu.
Pishi:
Limetetwa kwenu na bidada Sware Kaku. Asante sana mama naenda fanyia kazi hii
kitu.
Ramadan kareem
na siku njema kwetu sote In Sha Allaah.
Mmmh Mashaallah umenikumbusha mbali wwe mtoto. Hicho kitu sikajitia mdomoni katambo sana.
ReplyDeleteAsalaam Aleykum Madam.
ReplyDeleteHope swaum inapanda au sio.....
Aisee mbaazi za kupaka zinapanda sana na chapati...uwiiiii utamu wa aje sasa.
Naungana nawe mdau Sabrina. Jamani hii kitu upate na chapati hapo au wali wa nazi. mmmmmh mpaka mate yananitoka hapa.
DeleteAsante madam kwa kunikumbusha hii kitu
mmmmmmh
ReplyDeleteumenikumbusha kwetu walai..lol
ReplyDelete