Siku
ya 1:
Asubuhi kula matunda (lakini usile ndizi). Mchana chemsha kabichi, weka chumvi
kidogo na nyanya, chemsha na upate supu. Kula mchanganyiko huo na utajiona
umeshiba. Jioni kula tikiti maji na mbogamboga au kabichi uliyotengeneza
mchana.
Siku
ya 2:
Kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).
Mchana kula kabichi iliyochemshwa, tengeneza na kachumbari. Katika kabichi weka
chumvi, pilipili na mafuta ya olive. Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana
lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
Siku
ya 3: Kula mboga za majani na matunda, unaweza kuongeza
kiazi kitamu kimoja.
Siku
ya 4: Kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi
wakati wa asubuhi. Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya
kwanza, usiku rudia mlo wa mchana.
Siku
ya 5: Kula nyanya nne pamoja na samaki au kipande cha
kuku asubuhi. Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye
amechanganywa na nyanya. Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
Siku
ya 6: Unaweza kula chakula cha protini na mboga za
majani. Anza kwa kula kachumbari asubuhi. Mchana kula tambi kiasi na kipande
kidogo cha samaki. Usiku tengeneza supu ya kabichi.
Siku
ya 7: Anza kwa matunda na juisi. Mchana kula mboga za
majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
Kumbuka:
Unatakiwa kunywa maji kwa wingi. Usiendelee kwa muda mrefu.
TeamDiet
mpooo hapo. Hii kitu nimetumiwa na rafiki yangu Jully nikaona sio mbaya nishare
nanyi vipenzi nyangu sababu najua wanene tupo wengi hasaa na tunataka sana
kupungua. Diet hii niya mboga mboga na matunda.TeamDiet haya twende kazi.
Jully
my dear much respect mama.
Hapana chezea kabisa lazima upungue kwe mwendoo huu
ReplyDeleteTeamDiet tupo mama ila hii lazima chamoto ukione hahahaha chezea supu ya kabichi wewe
ReplyDeleteOverweight ni tatizo jamani. Tuzingatie maushauri haya.
ReplyDeleteUnene sio dili sema tu kujikondesha haraka haraka inakua shida sana kama hauna mavazi ya kutosha.Maana itabidi ununue pamba za kukutosha.
ReplyDeleteNimeipenda hii.
ReplyDeletewill try it
ReplyDeleteSafi
ReplyDeleteNaendelea kufanya leo siku ya 6 nimekula kachumbari nasubiri tambi da ila yataka moyo
ReplyDeleteJana afadhari kuliko ck zote nilizofanya
ReplyDelete