Haya
jongeeni kijiweni tuongezeane ujuzi wa mapishi. Angalia upishi wa KEBABU.
Mahitaji
1. Nyama ya kusaga kl 1
2. Kotmili/giligilani wengine huita kifungu
kimoja
3. Kitunguu maji vikubwa vitatu
4. Swaum kikubwa kimoja & tangawizi
5. Mikate ile ya elfu moja nunua miwili ama
mitatu
6. Chumvi kiasi
7. Binzali nyembamba na pilipili manga vilivyo
sagwa
8. Pili pili hoho kubwa moja
9. Mafuta ya kupikia
10. Ndimu
11. Mayai sita
Hatua
ya kwanza
Nyama
ya kababu hua aichemshwi habisa. Kumbuka nyama kama ina maji yakamua. Chukua
nyama yako weka kwenye chombo kisafi, tia chumvi, ndimu, unga wa binzari
nyembamba, kamulia na ndimu kisha tia pilipili manga, alafu changanya huo
mchanganyiko wako na uakikiche umechanganyika vizuri kabisa.
Hatua
ya pili
Katakata
vitunguu maji katika vipande vidogo vidogo kama vya sambusa vile, katakata pia
pili pili hoho zako katika mfumo huo huo pamoja na karoti, osha
kotmili/giligilani zako vizuri na ukamue maji alafu toa ile mizizi ya nyuma na
kisha katakata katika vipande vidogo vidogo, twanga swaum zako pamoja na
tangawizi na badala ya hapo tia katika mchanganyiko wako ule wa nyama.
Changanya mpaka uakikiche umechanganyika vizuri. Kuonja ruksa wapenzi iliuweze
jua kama vitu vyote vipo sawa au laa....
Hatua
ya tatu
Chukua
mikate yako toa ile nyama ya kati nikimaanisha ile nyama ya mkate nyeupe ule
upindo wa pembeni usiweke sababu ni mgumu na sio soft. Chambua mikate yako
vizuri kabisa na inyambue nyambue na uweke katika mchanganyiko wako wa nyama,
chukua mayai matatu uweke humo. Changanya vyote sasa kwa pamoja mpaka
uwakikiche vimechanganyika ipasavyo. Na baada ya hapo utafanya kama unakanda
unga wa ngano vilee na upate donge moja takatifu. Utaacha mchanganyiko wako kwa
mda wa kama dk 10 or 15 hivi ili viungo viweze kukolea kwa uzuri.
Hatua
ya nne na mwisho
Kata
vidonge vidodo vidogo ama upendavyo na kutengeneza style uipendayo, weka kwenye
chombo safi, vyunja mayainyako yale matatu yalio baki na uweke kwenye bakuli
toa vile viini vya ndani na ubaki na ute tu. Weka kikaangio chako jikoni na usiwe
na moto mkali, moto uwe wa wastani tu, mafuta yako yakisha pata moto chukua
kebabu zako tosa kwenye ule ute wa yai na uweke kwenye mafuta yakio jikoni na
utarudia kwa vyote viduara ulivyo fanya. Baada ya hapo vitakua tayari kwa
kuliwa. Ni tamuje sasa.....Very yummy waweza sukumia na chochote Wallah.
Cha
ziada
Wapenzi alafu ule mkate ulio utoa ule mgumu (upindo wa mkate)
hautupwi wapendwa. Unaufanya hivi; Ukaushe kwenye microwave ukauke vizuri usiungue.
Alafu utwange huo mkate wako mpaka upate unga unga. Baada ya kukata madonge
yako ya kebabu unaweka kwenye huo unga viliga viliga ukitoa unaweka kwenye ute
wa yai utafanya hivyo mara mbili na kasha utachoma.
By God yesterday nimejalibu pika KEBABU jamani jamani tamuje sasa.
ReplyDeleteUwiiii barikiwa mama uendeleee kutuletea vizuri vingine