Friday, August 03, 2012

Kachori

Maitaji ya pishi la kachori
o   Viazi (mbatata) vikubwa kiasi 5
o   Thomu na Tangawizi Kijiko 1 cha chakula
o   Chumvi Kijiko 1 cha chai
o   Pilipili ya kusaga kutegemea na unavyoipenda
o   Ndimu 1
o   Pilipili mboga (Pili pili hoho) 1
o   Karoti 1
o   Mafuta ya kupikia
o   Unga wa dengu au Ngano Kiasi

Namna ya kutayarisha na kupika
o   Chemsha viazi mpaka viwive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli.
o   Sukua karoti yako na mashine zile za mkono au unaweza kukata kata vipande vidogo vidogo, pia kata kata karoti yako vipande vidogo vidogo na uvichemshe kwa dakika moja au mbili tu.
o   Tia katika chombo viazi mbataba vyako na uviponde ponde mpaka viwe laini usiongeze maji. Unaweza tumia mwiko kusaga viazi nyako.
o   Saga thomu na tangawizi kisha changanya na viazi.
o   Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kisha uonje, unaweza kuongeza viungo kwa jinsi upendavyo.
o   Tengeneza magonge ya duara yenye ukubwa kiasi au unaweza tengeneza style yoyote upendayo na uyaweke kwenye sahani.
o   Chukua unga wako wa ngano au unga wa dengu utie kwenye bakuli na unganganye na maji, ujiji huu usiwe mzito sana na wala usiwe mwepesi sana unapendeza ukiwa size ya kati.
o   Bandika mafuta yako ya kula jikoni yakiwa kwenye karai na subili mafuta yapate moto.
o   Kuchua madonge yako uliyo yaandaa na ujatose kwenye uji uji wako wa ngano au uji uji wa dengu alfu toa na uyatie kwenye karai la mafuta subilia zichomeke na kubadilika rangi kidogo.
o   Toa kachori zako weka pembeni zijichuje mafuta na zipange vizuri kwenye sahani na zitakua tayari kwa kuliwa.


Dokezo:
 Kachori inaliwa wakati wowote na mtu yoyote pia sio lazima utie pili pili kama wewe sio mpenzi wa pili pili ni kitafunwa kizuri sana kwa kweli, kwanza soft hakiitaji nguvu wakati unakula.

Nawapenda sana na nawatakia Ramadhan Kareem.

2 comments:

  1. Asante Sis n ubalikiwe kwa kutuongezea ujuzi wa mapishi

    Mrs Nassib

    ReplyDelete