Monday, January 20, 2014

Mabadiliko baraza la mawaziri Tanzania


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa kuwateua mawaziri na manaibu waziri, kuziba nafasi zilizoachwa na mawaziri wanne waliojiuzulu na mmoja aliyefariki dunia hivi karibuni. Katika uteuzi huo Rais Kikwete amewateua mawaziri wapya wawili na manaibu waziri wapya wanane, huku akiwapandisha vyeo manaibu waziri wanne kuwa mawaziri kamili. Miongoni mwa mawaziri wapya ni pamoja na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dokta Asha-rose Migiro, ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria, huku Dk. Titus Kamani akiteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Waziri pekee aliyeachwa katika mabadiliko hayo ni aliyekuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa. Miongoni mwa manaibu waziri wapya ni pamoja na Juma Nkamia ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtangazaji, ambaye amepewa dhamana katika Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete yametokana na kujaza nafasi za mawaziri ambao walilazimika kujiuzulu baada ya ripoti ya bunge kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili kubaini kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utesaji na udhalilishaji vikidaiwa kutendwa na watekelezaji wa operesheni hiyo.

Ripoti hiyo iliwalazimisha waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kutangaza kujiuzulu, huku naye waziri wa mambo ya ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi kufuata mkondo huo bila kumwaacha waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Shamsi Vuai Nahodha, na Dr. Mathayo David Mathayo aliyekuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, kutokana na wizara zao kuhusika katika usimamizi wa operesheni hiyo ambayo iliwahusisha polisi, askari jeshi na walizni wa wanyamapori. Huku nafasi ya tano katika baraza hilo ikiachwa wazi na aliyekuwa waziri wa fedha, Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu.

Lupita Nyong'o WINS Best Supporting Actress at SAG Awards 2014

Congratulations to Lupita Nyong’o who is now a front runner for the Oscars.

The 12 Years a Slave actress picked up the award for Best Supporting Actress on Saturday 18th January 2014 at the Screen Actors Guild Awards in California, USA.

Congratulation Mama.

Thursday, January 09, 2014

African Sandals

zipo nyingi na design tofauti tofauti. Mzigo mpya umeingia
Hizo picha hapo juu ni design chache tu nilizo weka ila ukiitaji wasiliana nami.
 Mnunulie mkeo hata girl friend wako, nyumba ndogo yako, dada yako, mama yako, shangazi yako.
Jamani kuungana mkono ndio habariiiii ya mjini…….Lol
  
Bbm Pin: 29D24E8F
Skype: Amyna02
WhatsApp: +255 784 220 178

Karibuni sana kizuri kula na wenzio.

Tuesday, January 07, 2014

Number One Remix - Diamond Ft Davido

Hii ndio remix ya wimbo wa NUMBER ONE kutoka kwa Diamond feat Davido sasa ipo tayari na tena ndio hii hapa chini.
Enjoy