ASANTE
SANA MDAU ULIYESHEA...MUHIMU KUSOMA HII WADAU..
Ikiwa
siku ya chache baada ya tukio la kusikitisha la kuteketea moto kwa watu 9 wa
familia pale Buguruni, D'Salaam, vifuatavyo ni vitu vya kujifunza (few tips to
learn) inapotokea dharura ya moto ndani ya nyumba:
1. Kitu cha
muhimu ni kutoka nje salama haraka iwezekanavyo (as soon as possible).
2. Hakikisha
(ensure) kila siku mlango wa dharura (emergency exit) ya nyumba ni umekaa kwa
urahisi iwezekanvyo (as simple as possible). Kila mtu ajue funguo za milango ya
kutokea zinapowekwa, sio zinafichwa balaa. Have an ermegence exit whenever
possible.
3. Fahamu kwamba
ktk matukio mengi ya moto (in most cases) kinachoua ni moshi kabla ya moto,
hivyo ukiona dalili ya moshi hakikisha unakuwa na kitambaa kibichi cha
kujifunika puani na mdomoni, na kama moshi umeanza kuingia ulipo tambaa chini
(crawl down) sababu hewa ya uhai (oxygen) ina uzito (density) kubwa kuliko hewa
ya kifo (carbon monoxide) hivyo inakuwa imekandamizwa chini sentimita chache
kutoka kwenye sakafu (few centimeters from the floor). Hivyo tembea kwa
kutambaa.
4. Hakikisha
unawajulisha watu wote (Ensure you alert everybody) kama wamelala ili waweze
kutoka nje haraka.
5. Achana na fikra ya kuokoa vitu, ktk hatua hii
cha muhimu ni kuokoa uhai kwanza.
6. Kumbuka, muda ni kitu cha msingi, fanya haraka
iwezekanavyo (quick as possible) katika kujiokoa na kuokoa wengine.
7. Ni muhimu
nyumba zetu kuziwekea kiashiria moshi (smoke detectors) na pia kizima moto
(fire extinguishers). Kugundua haraka (early detection) ya moto ni muhimu sana
ili kuweza kuudhibiti kirahisi. Smoke detector ni mashine ya elektroniki ambayo
inagundua moshi ktk hatua ya mwanzo kabisa na itapiga kelele (alarm) kwa sauti
ya juu, itakusaidia kuamka hata kama upo usingizini na kuweza kujiokoa na
kuokoa wengine na kuuzima moto kabla hujashika kasi.
Shukrani na sambaza ujumbe
huu kwa wengine
Asante mpenzi kwa kutujuza. Barikiwa sana ndugu
ReplyDeleteasante kwa kushare nasi
ReplyDelete