Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia
kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa
mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro Brazil 06/04/2014.
Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya
pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto
wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.
Katika mechi ya fainali Tanzania iliibanjua Burundi iliyokuwa ikipewa
nafasi kubwa ya kulinyakua kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3-1 huku mchezaji
kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa
nyota wa mchezo. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tanzania ilikuwa
ikiongoza kwa magoli 2-0. Kipindi cha pili iliongeza bao la tatu. Burundi
iliweza kupata bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika nne mpira
kumalizika.
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata
kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino
na Argentina.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa
michuano hii ya kombe la dunia.
Hii ilikuwa mara
ya Pili kwa timu ya Tanzania kutinga fainali za michuano hiyo ya dunia kwa
watoto wa mitaani inayofanyika siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia
kuanza mwezi Juni. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii kule
Durban Afrika Kusini mwaka 2010 Tanzania ilifungwa na India katika fainali. Watanzania
tunaweza sana. Mungu awaongoze vijana wetu mzidi fanya vyema zaidi na zaidi.
HONGERENI VIJANA NA PIA MSILEWE SIFA.
ReplyDeleteKAZENI BUTI TANZANIA TUNA TAKA MABADILIKO
Hawa vijana ni hazina kubwa. Wafunzwe vyema ili waje kuchezea timu ya taifa...TFF embu waangalieni hawa vijana kwa jicho la tatu
ReplyDelete