Serikali
imetangaza uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato cha nne ya 2012. Uamuzi huo
umetangazwa mapema leo bungeni na Waziri William Lukuvi, kwa niaba ya Waziri
Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu iliyokuwa inachunguza kuhusu
matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa kwa utaratibu tofauti na
uliokuwa unatumika zamani.
Tetesi
za awali zilieleza kwamba matokeo hayo yalipangwa kwa kuzingatia madaraja haya
hapa chini, japo Baraza la Mitihani lilikanusha baadaye kwa kusema kuwa taarifa
hizo hazikuwa za kweli.
A
= 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-
Tume
ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa madaraja tofauti na uataratibu wa awali.
Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa hayatatumika tena mpaka yaje yaliyopangwa
upya. HakiElimu itatoa taarifa rasmi baadaye kuhusu uamuzi huu wa serikali.
Soma
zaidi status yao http://www.facebook.com/#!/pages/National-Examination-Council-of-Tanzania-NECTA/101411643286736
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment