Wednesday, February 08, 2012

Matokeo Kidato cha nne 2011

Wapendwa wadau wa love2know-amynag. Matokeo ya kidoto cha nne ndio hayo yametoka. Kama mtoto wako, mdogo wako, ndugu yako, rafiki yako, jirani yako amemaliza kidato cha nne mwaka jana. Fungua hii link kuona matokeo zaidi http://196.44.162.14/necta2011/olevel.htm


Kama mtoto wako amefail tafadhali usimvunje moyo ama kumsema sana mpaka akajiona mkosaji ndani ya dunia hii, mtie moyo, mshauri na ata ikiwezekana aweze kuludia tena mtihani. 


Pongezi kwa wote walio fanya vizuri. Kwa wale walio fanya vibaya tafadhali msifunjike mioyo bado mna nafasi ya kufanya vizuri zaidi.


Nawapenda sana

8 comments:

  1. Umesema ukweli Amyna.
    tuwatie nguvu ndugu zetu kwani kuwasema sio ndio kutabadilisha matokeo na kua mazuri. tuwape nafasi nyingine wa kuwatia nguvu zaidi ya kuweza kufanya vizuri.

    Ila hao watoto nao wajue kua maisha ya sasa ni magumu wanapaswa kusoma sana tena kwa bidii ili waweze kufanya vizuri na kuwatia moyo wazazi au walezi wao wanao walipia ada pia inatengeneza CV nzuri hata kwao wao wenyewe pia.

    Asante Amyna kwa kutufahamisha juu ya hili. Ubalikiwe mama

    ReplyDelete
  2. Jamani watoto wengine wameshindikana kaandika wimbo katika booklet lake. Ivi kweli mzazi anapoteza pesa zake ukasome afu unafanya utumbo huo....

    Vijana tubadilike jamani tuwaoneeni huruma wazazi na walezi wetu wanao tulipia ada maisha magumu n wanatafuta pesa kwa tabu ili watoto wao tusome.

    Ammy Ubalikiwe mpnz kwa kutufahamisha.

    Faraja.

    ReplyDelete
  3. Wwe binti unaweka hiyo kwani sisi atujui wedsite ya NECTA afu ndio mashauzi.

    Shuda Boy.

    ReplyDelete
  4. Shuda Boy najua unajua ila napenda ujue zaidi. Pia naomba nikusahihishe kidogo sio "wedsite" ni "WEBSITE" sawa kaka.

    ReplyDelete
  5. Kipindi hiki ndio utasikia matukio mengi ya watoto kujinyonga baada ya kusemwa na wazazi kwa matokeo mabaya. Tuwapeni nafasi nyingine ndugu zetu kwani mfanya kosa sio kosa ila mludia kosa ndio kosa. Kuwasema ni muhimu ili wajue kama walicho fanya ni kibaya kwa maendeleo yao wenyewe ila usimseme kupitiliza ampaka wakajiona hawafai hapa duniani.

    Mama Tunu

    ReplyDelete
  6. Ammy u know its really pain. Me hapa ninapo kaa kuna bint amemaliza form 4 cku ambayo matokeo yametoka baada ya siku mbili kajifungua mtoto tena wa kiume.

    Sasa jamani mtoto kama huyu unamfanyaje? Kweli usimseme kama unavyi sema? Mzazi wake kapoteza pesa ngapi kumsomesha akiwa na mategemeo mtoto wake atafanya vizuri. Sasa vizuri yake kamletea mjukuu. Basi matokeo yametoka walau awe amefanya vizuri.... Kamletea mzazi wake div 4 ya mwisho hata uwalimu huchukuliwi na mjukuu juu.

    Watoto hasa wa kike badilikeni jamani mna waumiza wazazi wenu. Now dayz maisha magumu wazazi wana tafuta pesa kwa nguvu ili kufanya family yake iishi vizuri. Lakini baazi yako ndio wanafanya madudu kama haya..

    ReplyDelete
  7. Thankx Amyna for the news

    ReplyDelete
  8. Uyo mtoto kashindikana na atakua kamaliza shule na mimba. Jamani mbona watoto wa cku hizi wana balaa

    ReplyDelete