Uchaguzi
Mkuu Tanzania Oktoba 25, 2015.
Namuomba
sana Mungu wangu (Allah) Uchaguzi upite salama bila ya machafuko ya aina yoyote
na wagombea wote napenda wakumbuke kua Siasa sio ajila na cheo ni dhamana, sasa
haya mambo ya kuto kukubali matokeo kama upemeshidwa ndio nini?? ama
tukueleweje?? Kuna msema wa wahenga walisema “asie kubali kushindwa sio
mshindani”.
Yote
kwa yote watanzania wenzangu tusikubali kushawishika kuvuruga amani yetu maana
amani ikipotea ni ngumu sana kurudi tena, embu tuone Inchi za wenzetu watu
wanavyoangaika, mauwaji ya kila uchao, watu hawali wakashiba, hawafanyi
maendeleo ya aina yoyote kutwa kucha ni kukimbia tu. Jamani tulindeni amani
yetu kwani ni hadhina kubwa sana sana.
Binafsi
mimi sipo upande wa chama chochote na nimechagua Raisi, Mbunge na Diwani
kutokana na sera zao, utendaji kazi wao n.k sijachangua kwa kufuata mkumbo wa
mtu.
Watanzania
tuache tabia ya kujitolea matokeo wenyewe maana kila mtu anatoa matokeo yake
utazani yeye ndio msemaji wa tume matokeo yake watu wanakinzana huko mitaani na
mitandaoni, tushaambiwa tutulie tume inafanya kazi yake na tume ndio chombo
pekee kinakachotoa matokeo ya walio pita kwenye uchaguzi.
Mungu(Allah)
wabariki washindi wote ambao mpaka sasa wameshatangwazwa na tume na
wanaoendelea kutangazwa na tume, Ya Allah uwajaze busara, imani, upendo miyooni
mwao waweze kulitumikia Taifa hili kwa mioyo yao yote bila ya kufanya matendo
ya kifisadi, watimize ahadi zao walito zisema kwa wanainchi wao, washirikiane
na wanainchi katika kuleta maendeleo ya maeneo yao na Taifa kwa ujumla,
Ukawajaze busara na uwape muongozo ulio tukuka katika kufanya maamuzi yoyote
yanayo usu masaili ya Taifa hili...wote tusema Ameeeen.
Tudumisheni
Amani, Upendo na Mshikamano.
Naipenda
Tanzania yangu, Nawapenda Watanzania wenzangu wote.
Mungu
ibariki Tanzania na Mungu tubariki Watanzania wote.