Siku ya familia duniani huadhimishwa kila mwaka May 15, na kauli mbia ya mwaka huu ni “UWAJIBIKAJI SAWA KATIKA MAJUKUMU: MSINGI WA FAMILIA BORA.
Wadau wote wa AmynaG Blog tukaeni na familia zetu kuchambua na kupanga mikakati ya maendeleo endelevu katika familia zetu. Tuzithamini, tuzipende, tuzieshimu na tufanyie familia zetu mambo yote muhimu ambayo yanafaa na yanastahili kuzifanyia familia zetu.
Wana familia upendo ndio msingi muhimu wa kudumisha amani na maendeleo ndani ya familia na taifa kwa Ujumla.
Picha zote hapo juu ni baadhi ya wanafamilia ya Gama.
Mungu zibariki kila Familia duniani, Mungu zibariki Familia zote za Tanzania....Amini.